• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Research Journal Articles
    • Department of Education
    • View Item
    •   Repository Home
    • Research Journal Articles
    • Department of Education
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Ubadili Maana katika Leksia za Kîîtharaka: Mtazamo wa Kifonolojia na Kimofolojia

    Thumbnail
    View/Open
    1667414754706_Mwembu, Mugambi & M’Ngaruthi (2022) - EAJSS 2 Article.pdf (341.0Kb)
    Date
    2022-09
    Author
    Kimathi Mwembu
    Allan Mugambi
    Timothy K M’Ngaruthi
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Makala haya yanalenga kubainisha jinsi ubadili katika vitamkwa na mofu unavyoathiri maana ya leksia katika Kîîtharaka. Maana katika leksia hutegemea kipengele cha kiisimu na vile vile kile cha kijamii ili ieleweke vilivyo. Katika hali hii, mabadiliko ya kifonolojia, kimofolojia, pamoja na kileksia yanayoathiri maana yameangaziwa. Data ya kimsingi kutoka wazungumzaji asilia wa Kîîtharaka, imechanganuliwa kwa kutumia nadharia ya Leksika-Pragmantiki. Makala haya yanabainisha ubadili wa kifonolojia pamoja na kimofolojia ambao huchangia katika kuibuka kwa maana fulani katika leksia za Kîîtharaka. Makala haya yanabainisha kwamba maana katika leksia za Kîîtharaka hutegemea kwa njia moja au nyingine mabadiliko yanayohusisha usilimisho, kuimarika na kudhoofika kwa fonimu, uchopekaji, uyeyushaji, hapololojia, kanuni ya Dahl na Ganda. Aidha, ubadili unaoathiri maumbo ya mofu huchangia pakubwa kutokea kwa maana katika leksia. Mofu za ngeli, ukanusho na uambishaji ni miongoni mwa zile ambazo zimebainika kuathiriwa na ubadili, ambao huzua maana fulani. Makala haya yanahitimisha kwamba, maana ya leksia huwa na misingi yake katika kiwango cha fonimu na mofimu zinazotumika kuunda neno. Pia, kuna mwingiliano baina ya maana kimatumizi na maana kimuktadha wa leksia.
    URI
    http://repository.tharaka.ac.ke/xmlui/handle/1/4013
    Collections
    • Department of Education [38]

    Tharaka University copyright © 2020  Repository
    Contact Us | Send Feedback
    Designed by
    TUN Library
     

    TUN
     

     

    Browse

    All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Tharaka University copyright © 2020  Repository
    Contact Us | Send Feedback
    Designed by
    TUN Library
     

    TUN